Jinsi ya kujenga tabia ya kupenda kujisomea - hamasisha

Thursday, May 18, 2017

Jinsi ya kujenga tabia ya kupenda kujisomea









  • jiambatanishe na watu wanaopenda kusoma vitabu






waswahili wanasema chuma hunoa chuma , kujiambatanisha na watu walio endelea kuna kujenga kuwa na mtazamo endelevu . kuwa na marafiki wapenzi wa vitabu kuna kufanya uwe na taarifa kuhusiana na vitabu tofauti. utapata ile shahuku ya kutaka kujua vitu au kujifunza vitu vingi .

  • anza na vitabu vidogo na vyepesi kuelewa

vitabu vidogo havimfanyi mtu kuwa mvivu  , ukianza na vitabu vikubwa kama wewe si msomaji mzoefu vina kupelekea kukifu kujisomea. huenda ukawa unakipenda ila kitakuchukua mda kukimaliza . chagua kitabu chepesi kwa mantiki ya kwamba kitabu hiko kiwe na lugha nyepesi, uchache wa mafumbo na kiwe kina jieleza chenyenyewe

  • panga mipango na mda wa kujisomea

kujijengea mda maalum wa kujisomea na mpango . mfano ; 'unanunua kitabu na kukigawa ,kila siku unajukumu la kumaliza ukurasa mmoja' ukiwa ni msomi mgeni unatakiwa kutenga mda ambao unaona huto pata usumbufu wa aina yoyote.hii itasaidia wewe kufika hatua fulani katika kujenga tabia ya kujisomea. unashauriwa kutembea na kitabu chako endapo ukipata mda basi utaendelea na kusoma

  • tafuta mazingira sahihi kwa kujisomea

mazingira na mda ni mambo muhimu katika kutafuta umakini . kusoma kwa ujumla anatakiwa msomaji atafute mahali  penye utulivu wa hali ya juu .

usemi wa waafrika hawapendi kujisoma , kusoma vitabu ni tabia ya kigeni si sahihi bali kupenda kusoma au kutokusoma ni tabia ambayo mtu binafsi anaweza kujijengea ua kuacha pia. vitabu vinapanua uwezo wa mtu kuelewa na kutafakari mambo . mfano elimu za kihistoria, hadithi za kweli, tafakari za kisaikolojia na vinginevyo 

No comments:

Post a Comment