Wahenga wanasema acha kazi uone kazi kupata kazi, kwanini mtu aache kazi wakati ndio njia kuu ya kujiingizia kipato?, ukiuliza swali hili utapata majibu mengi mno. Kukosa amani sehemu ya kazi kwa misuguano ya hapa na pale, kufanya kazi nyingi kupita uwezo, masilahi, mgandamizo mkubwa kutoka kwa viongozi, na mengineyo. Je unadhani ukiacha kazi itakuwa suluhisho la matatizo au ndio mwanzo wa matatizo mengi ambayo hujui yataisha lini. Ukiwa na kazi iwe kwenye mkataba au la unawajibika kufanya kazi kwa juhudi zako zote kwa kile ulicho kubaliana na mkubwa wako wa kazi. Kwani taratibu wa kazi upo vilevile sehemu zote .
Usiwaze ugumu wa Kazi
Ukimtafakari bata basi kumla itakuwa Kazi. Ugumu wa Kazi usikuzuie wewe kufanya Kazi. Unachotakiwa ni kuweka mipango mikakati na kukubaliana na hali .mda Fulani nafanya hichi na nikimaliza nafanya kile. Hata kama Kazi iwe ngumu kiasi gani unatakiwa ujifunze kumaliza Kazi moja ndipo ufanye ya pili. Ukishamaliza usichoke kujipongeza kwamaana itakupa moyo wa kufanya nyengine.
tengeneza mlengo binafsi
Lazima nifike kule. Lazima ni malize hapa Kwanza na pale ili nifike kule. Kabla hujaingia ofisini tambua unaenda kufanya nini siku hiyo. Jipangie wakati wa kufanya Kazi mfano: mda huu mpaka mda huu natakiwa kufanya hiki na hiki. Usipojua unachoenda kufanya kazini basi tambua utafanya Kazi nyingi bila mpangilio na itakupelekea kuchoka sana.
Usipigane kila vita
Misuguano ipo kila sehemu Ili ujifunze ,basi haina budi kukubali kukupambana na vikwazo.mahali pakazi kuna watu wengi wenye tabia tofauti. Ila cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuchambua kila aina ya maneno na mishale. Ukikwepa vita visivyo na msingi hautopoteza mda wako. Chagua vita vyako si kila mtu wa kubishana nae utaishia kupata mawazo na uchovu usio na mantiki.
Jali mda wako na fanya Kazi kwa bidii
kazi na mda ni vitu vinavyorandana, ukitunza mda wako na kufanya kile kilicho kuleta kazini na kuweka bidii katika kila unachofanya maisha yako hayatokuwa magumu. hamna kitu kizuri kama kuwahi kazini ,itakufanya kupata mda wa kupumzika na kufanya kazi akili ikiwa imetulia.
Tunza tabasamu Lako
furaha ni kitu kizuri zaidi kwa kila mtu , na hii furaha huwezipewa na mtu. katika maisha mtazamo hasi huondoa huzuni kwakila mtu. jaribu kuwa na mtazamo chanya , inasaidia kuondoa mawazo ambayo yatakupelekea kupoteza furaha. hata ukiwa unazongwa na matatizo kutoka nyumbani haipaswi kumshirikisha kila mtu katika eneo lako la kazi.
Jiamini na tambua haki zako
kuwa na imani na kila unachokifanya kunaanza na kujua nini unafanya mahali gani unataka kufika na unachokifanya,kujiamini kuna kutengenezea mipaka, kutambua haki zako haitoshi unatakiwa kuwa na ujasiri wa kutetea haki zako pia.
No comments:
Post a Comment