Umuhimu wa "folic acid" kwa mama mjamzito - hamasisha

Wednesday, August 9, 2017

Umuhimu wa "folic acid" kwa mama mjamzito

Folic acid ( vitamin B) , imetengenezwa Katika mchanganyiko wa virutubisho ndani ya vyakula asilia na matunda inayounda kidonge ambacho kinapatikana mahospitalini pamoja na maduka ya dawa ,  uzuri wake folic acid unaweza kupata ukila vyakula kama dagaa, maharagwe, mboga za majani, njegere, matunda, mayai  ya kuchemsha na vinginevyo . Folic acid husaidia katika umbaji wa viungo vya mtoto akiwa tumboni

Matokeo ya ukosefu wa folic acid

  • Mama kupungukiwa na damu
  • Kutoka kwa mimba au kuzaa kabla ya wakati
  • Mtoto Kuzaliwa na ulemavu
  • Mtoto kupatwa na magonjwa kama kichwa kuwa kikubwa, mdomo wazi, mgongo wazi

Mama anaenyonyesha anashauriwa kupendelea vyakula vilivyo na folic acid pamoja na mama anaetafuta mimba.