Umakini katika kuajiri - hamasisha

Sunday, July 2, 2017

Umakini katika kuajiri

Mahusiano ya mfanyabiashara na mwajiriwa wake kaitika biashara ndio yatakayo mfanya mteja kutoa maana ya huduma yao kwanamna ya ukarimu na ufasaha. Wasomi wanasema ukimjali mfanyakazi wako utakuwa umemjali na mteja wako. Mfanyakazi wako katika Biashara ni mtu anaekuunganisha wewe kiongozi au mfanyabiashara na mteja wako mlengwa. Achana na uhamasishaji kwa namna ya vizawadi bali upendo wako ndio utakao ashiria umakini wako kati yako na mfanyakazi wako kwa mteja. Umakini katika kuajiri , unakuta mfanyabishara umejijenga na kuwekeza katika Biashara yako zaidi  ya miaka miwili  na inakuja kutenguliwa na mtu ambaye umemuajiri ndani ya miezi sita kwa kukosa umakini katika kuajiri.

Historia ya mwajiriwa

Ndege wanaofanana huruka pamoja, maana ya kuwa ukimuajiri mtu ambaye hamrandani kitabia hata kiimani pia basi kutakuwa na chembechembe za kuto kuendana katika utendaji wa Kazi. Historia ya mwajiriwa sio rahisi ila watu wengi au wafanyabiashara hudharau Yale majina ya wadhamini , wale wadhamini wapo pale kwaajiri ya kukuunganisha wewe na mfanyakazi wako kiusalama na ni kwa faida yako.

Uaminifu na Ufanisi

 kupata mfanyakazi mwaminifu ni jambo la kumshukuru Mungu kwa maana binaadamu huangalia masilahi yake kwanza kutokana na majukumu yanayomuelemea au tamaa , kwanini mfanyakazi akuibie ?, yamkini inawezekana ukawa wewe ndo tatizo , miashahara isiyo na masilahi au kutokuwa na upendo nae. silazima umpe pesa au kumkopesha bali kuhusika katika maisha yake hata theluthi. unaweza ukapata mtu muaminifu ila akakosa ufanisi katika anachofanya , ufanisi kwa namna ya mapenzi na anachofanya , ukishakuwa na upendo na anachofanya ubunifu na mawazo ya kimaendeleo pia hufuata .

Mahusiano na Mipaka

kwa wafanya biashara wadogo au hata wakubwa waliowengi huamini kwamba mtu aliekaribu nawe iwe rafiki au ndugu hawezi kukufanyia udhalimu katika sekta unao iheshimu kama ya biashara.  ushungu au uzito wa hali anaijua aliepitia, sekta za fedha zinahitaji umakini wa hali ya juu, mipaka na heshima hujengwa na mwenyeji kisha mgeni hufuata nyayo za mwenyeji wake . ukiwa na matumizi mabovu ,kukosa mikakati ya utunzaji rekodi za biashara , mfanyakazi wako hawezi kufanya nje ya hayo. mipaka na sheria ndio mikakati mizuri ya kutunza mahusiano kati ya mwajiri na mwajiriwa.