Fursa na upendeleo havitokei kwenye maisha kirahisi; inategemea na uzito au thamani uliyojijengea na ndiyo inayowapa sababu ya kukuchagua wewe. katika maisha ya binaadamu anapitia ngazi tofauti na katika hizo ngazi anakutana na watu wengi wa tofauti walio katika kila ngazi nakukutana na fursa tofauti au changamoto zitakazo mjenga kiakili. Katika mchanganyiko wa watu utakutana na vikundi na taasis tofauti na zote hizi ni kwaajili ya kuleta umoja na maendeleo katika jamii. Mchango wako katika kuendeleza au kuleta maendeleo Fulani ndiyo thamani yako. Thamani yako kwao inaletwa nakile unachokipindua kutoka kwenye hasi.
Jinsi ya kutengeneza thamani yako
Fanya vitu sahihi
jijengee taratibu ya kufanya vitu sahihi na vya kimaendeleo jiambatanishe na vikundi au taasisi za waleta mabadiliko. Ukiwa shule au mtaani hakikisha unaleta mageuzi ili mambo yaende mlama. Heshimu na jali unachofanya , fanya kwa moyo wako. Kuwa na misimamo na neno Lako. Heshimu watu wote na kila wanachokifanya. Jisheshimu , heshimu muda wako na kile unachotaka kufanya. Hii itakutengenezea mipaka kwa watu wasio sahihi kwako.
Wekeza
ukiongelea hili watu wanahisi ni kufanya Biashara au kunua hisa Fulani. Kuweke ni kutia nguvu na akili yako katika kujenga kitu Fulani. Kama wewe ni mwanamichezo wekeza katika mazoezi, nunua vifaa vizuri vya mazoezi heshimu wasimamizi wako. Jitoe kwa moyo wako wote yamkini faida hauto iona ila unajijengea uimala katika fani au kusudi Fulani.
Kuwa na mlengo
jiamini na uamini mlengo wako. Fanya vitu vyenye mchango chango katika malengo yake. Jijenge kupitia kusoma taarifa tofauti za watu waliofanikiwa. Jiungamanishe na watu waliofanikiwa. Wekeza mda wako kwa kujifunza na kujifunza kwa bidii vitu tofauti.
Faida za kutengeneza thamani yako katika jamii
Kivutio kwa mahusiano chanya
ukieleweka watu watakuelewa, ukiwa mtu mwenye haiba chanya utapendwa na watu. Watu watapenda kujifunza kwako na kushirikia na wewe katika mipango ya kimaendeleo
Kuaminiwa na kupata fursa:
ukionesha moyo katika Kazi zako na kupenda kila unachofanya katika ubora stahiki lazima watu watakuamini katika hiyo fani na ndipo milango ya fursa itafunguka.
Kutengeneza Mtandao na watu waliofanikiwa
Chuma hunoa Chuma, watu waliofanikiwa wanapenda kujiambatanisha na watu wenye vitu vinavyoweza kuwaongezea katika njia moja au nyingine. Ukiwa na thamani na kuthamini unachofanya lazima uaminike na kujipatia marafiki wenye mtazamo sawa