Pengine haujawahi kujiuliza swali hili ila ni swali amabalo unapaswa kujiuliza mara baada ya kuamua kukupa nafasi kwenye moyo wake kumbuka daima moyo mmoja hauwezi penda wawili.
Hivyo kila utambuapo ama kujiuliza swali hili iulize tena nafsi yako kama na yenyewe imemchagua kama alivyokuchagua wewe lengo ni kutokuja kumuumiza baadae
Tambua akilia kwa ajili yako ujue alimaanisha kulia na kama utamliza kwa makusudi tambua ipo siku nawe utakuja lizwa kama ulivyo mliza akikuchagua mliwaze usimlize.
Jiulize kwa nini ulimuambia kwa mzaha wampenda kweli kumbe haukua hivyo na yeye akaufungua moyo wake kupokea maneno yako mazuri na kulifanya tabasamu lako linawili zaidi na liwezuri kwake,usifanyemzaha nahisia za mtu mpende akikupenda.
Na usijaribu kujaji ama kuchukulia eti ni mahala gani mlikutana na kumuelezea hisia zako na yeye bila hatakujali akakubali yale ambayo ungemwambia na kukufanya uwe mwenye furaha wakati wote hasa ukizingatia ni mara ya kwanza kwako kumuelezea hisia zako na yeye bila hata chembe ya woga akakubali na kukuchagua wewe uwe msiri wake jiulize kwa nini alikuchagua huenda akawa anamengi anayajua kuhusu wewe lakini mwenyewe hujui.
Usijaribu kucheza na hisia zake mfanyie kile ambacho kitampa furaha,amani na upendo wake uzidi kwako na si mbaya kama siku moja ukajaribu kumrudia na zawadi kisha utajua kwa nini alikuachugua wewe na si yule mwengine.
Tambua penzi lake ni zaidi ya ufikiriavyo jitoe kwa ajili yake kama alivyojitoa kwa ajili yako mheshimu,mthamini mpe kile akipendacho kwa wakati,usisite kufanya hvyo ni kujenga thamani yako zaidi ya vile ufikiriavyo.
Elewa alikupenda kwa madhaifu yako mpende kwa madhaifu yake mtafika pamoja safari yenu ya mahaba na pendo la kweli ndio litakua vazi lenu daima .
No comments:
Post a Comment