Eda julias mwasposya mkazi wa njia panda ya segerea 29. Mimi ni mjane mwenye watoto wawili , David na Emanuel. Nina wapenda sana wanangu ila nina shindwa kuwatimizia mahitaji Yao kutokana na hali ya kifedha niliyonayo. Sina mama wala baba , Katika huu mchakamchaka nipo pekeangu yamkini utaelewa machungu na tabu nilizopitia msaada wako ndio tumaini langu. Nilizaliwa jijini mbeya tunduma. Mama yangu mzazi aliondoka duniani nikiwa na miaka miwili sikupata fursa ya kupata malezi yake Mungu ailaze roho yake mahali pema . Nilipoanza shule baba yangu akaiaga Dunia .nikiwa Chini ya usimamizi wa mama yangu wa kambo pamoja na baba mdogo maisha yangu Hayakuwa mazuri. sikupata malezi Ambayo mtoto wa umri wangu alitakiwa kupata. Mbadala niliishia kutanga tanga na kufanya kazi za ndani Katika hali ngumu zaidi . Maisha yangu yote sikuwa na ndoto labda huenda ntakuwa daktari au hata muuguzi hapana ndoto yangu kuu ilikuwa nikuomba huenda asubuhi itapambazuka na tabasamu jipya. Kwabahati nzuri malango ya kanisa yalikuwa kimbilio langu. Sitosahau mchungaji wa kanisa moja aliagiza waumini wake wanipe sadaka. Nilifarijika japo faraja ya mda mfupi. Mchungaji alinifanyia mchakato wa kurudi nyumbani kwetu mahala nilipozaliwa. Nilianza kufanya kazi saloon . Baada ya siku kadhaa kupita nilipatwa na tatizo. Nyumba yetu iliungua na sikubahatika kutoka na kitu chochote niliumia sana kwa nini mimi tu . Nilitaka kunywa sumu nipotee duniani kabisa kwa msaada wa watu sikufanikiwa. Ndoa yangu haikuwa mpango wangu kwa mda ule .njama za mama yangu wa kambo ila kwa bahati nzuri Mungu alinibariki mume mwema Kisha tukahamia Zambia . Mungu alinibariki na mtoto wangu wa Kwanza David . Tukiwa Katika maisha yetu ya kifamilia tulipata mgeni Ambaye nishemeji yangu. Cha kushangaza ujio wake haukuwa na matunda mema. Shemeji yangu nilimshuhudua akimkaba mume wangu mpaka mauti Sitosahau maana nilipiga kelele kwaajili ya msaada na mume wangu alilalamika " mama nisaidie , Mali zinaniua" nilipatwa na uchungu sana .watu waliniondoa pale na kudai anatibiwa kumbe mauti yalisha mkuta. Nikiangalia nipo ugenini nchi ya watu moyo wangu ulisononeka sana Nikakumbuka yaliyopita Sema sikuwa na jinsi. Mwili wa marehemu mume wangu ulisafirishwa mpaka nakonde Zambia. Baada ya mazishi kikao kiliitishwa ndipo ndugu wa mume wangu walinishtumu na kudai nilimuua marehemu baba David na kuita watu ili wammalizie ndugu Yake. Huwezi amini nilipigwa sana ndipo mke wa muuaji alinichukua na kunificha Chooni. Polisi walikuja na kunichukua na nikalala Polisi usiku ulikuwa mrefu sana. Mimi eda Leo nalala police tena ugenini, usilo lijua ni kama usiku wa kiza. Nilirudi kwa mama yangu wa kambo bali alinikataa na kusita kunikaribisha Kwake akidai huenda ndugu wa marehemu mume wangu wakaja. Nilikimbilia kwa bibi yangu huku kesi inaunguruma hakimu wa Zambia alinisaidia kupata haki yangu . Niliamua kukimbilia dar es salaam ndipo niligundua nina ujauzito wa Emanuel. Nilijaribu kuomba madaktari wanitoe ikashindikana. Nikazaa mtoto wangu wa kiume mzuri . Baada ya mda ikagundulika mtoto anatatizo LA kichwa kuwa kikubwa . Zunguka huku na huku kuomba msaada mtoto akafanyiwa oparetion ya kichwa. Maisha yamekuwa magumu sana Kwangu. Ndugu zangu hawana msaada. Nipo mimi na wanangu. Naomba msaada wenu mungu mwenyezi atufanyie wepesi wa maisha
Tunaomba msaada wenu +255768994609
Mungu awabariki!
🙏🙏🙏🙏🙏🤦♀️😭Amina
ReplyDelete