IFAHAMU SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI - hamasisha

Wednesday, August 23, 2017

IFAHAMU SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Asilimia kubwa ya saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa virusi wajulikanao kama human papilloma virus  (HPV) kwa mujibu wa tafiti. Mlango wa kizazi ni eneo katika mwili ambalo lipo katikati ya uke na tumbo la uzazi yenye urefu wa sentimita 2 - 3  ambayo hupitisha mbegu, hedhi na mtoto. 

Napataje kansa ya kizazi?

  • Umri
  • Kuwa na mahusiano na wanaume wengi
  • Uvutaji wa sigara
  • Ukosefu wa Kinga mwilini
  • Kuwa na mwanaume mwenye wanawake wengi
  • Kujihusisha na ngono katika umri mdogo


Ntajuaje sasa?

  • Kutokwa na damu nje ya hedhi 
  • Kupatwa na hedhi ya mda mrefu
  • Kupoteza uzito
  • Kutokwa na damu baada au ukiwa unajamiana
  • Uchovu
  • Maumivu kwenye nyonga na chini ya kitovu
  • Kutokwa na uchafu usio wa kawaida


Virusi vya human papilloma vinaenezwa na ngono zembe. kwa bahati nzuri wataalamu wamefanya utafiti kusiana na hii cancer na matibabu yapo (dawa au drip, mionzi na upasuaji). Tunashauriwa kufanya uchunguzi mapema kuepuka athari   kubwa zaidi. Uchunguzi ni bure kwa mujibu wa sheria umri wa miaka 25 na kuendelea

Source Tanzania cancer society
#stopcancer