Maendeleo binafsi na uboreshaji wa maisha yako kifedha
Kwa maisha ya mtu wa kawaida akiba ni ngao ya maendeleo yake kwa maana apatapo pesa kuna matumizi binafsi na familia kwahiyo huyu mtanzania akikwatua na kuweka pembeni akiba yake kwa malengo fulani bila kupandisha kiwango kwa matumizi yake ataiona Pesa . Huwezi kujenga kwa siku moja kupitia mshahara wa 200,000tsh. Bado hujatoa matumizi na dharura.
Ulinzi.
Pindi unapopata dharura akiba inakuwa mkombozi mbadala wa kukopa . Matatizo hayana taarifa wala majira akiba itakuepusha wewe kutokukopa mikopo mikubwa kutatulia matatizo. Kuna njia mbadala ya kuweka akiba njia ya kudunduliiza, unaweza ukajiunga na insurance kwa ajiri na afya na mengineyo.
uwekezaji
Kipaumbele cha Kwanza cha kuongeza kipato ni kupitia uwekezaji ila ntaanzaje kuweza kwenye Biashara bila mtaji? Ukitaka kuwekeza tafakari na kuchanganua mpango wa Biashara kisha weka mlengo. Akiba huingia pale unahitaji kianzio. Hata kununua hisa inakuhitaji uwe na Pesa! Ntapataje Pesa , "akiba"
No comments:
Post a Comment