UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE WALEMAVU NI ZAIDI - hamasisha

Wednesday, February 22, 2017

UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE WALEMAVU NI ZAIDI

Kutothaminika mwanamke katika jamii na kuonekana hawana mchango wowote ni changamoto ambayo tunayoishi nayo katika mazingira yetu japo serikali na taasisi binafsi zimekuwa zikitoa elimu kuhusu haki za wanawake na kupigania sheria inayomtetea mwanamke
unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke mlemavu umekuwa Mara mbili zaidi ya mwanamke asie na ulemavu. Ubakaji,unyanyasaji,
uzaririshaji na unyang'anyi ni vitendo wanavyopitia katika maisha yao bila kupata mtetezi au namna ya kufika sehemu watakayo pata haki zao.   



    Elimu na Afya

Kutokana na ulemavu walionao, wanawake Hawa haswa wale wanaoishi vijijini imekuwa changamoto kupata elimu mbalimbali kama lugha ya alama kwa upande wa viziwi. Kukosa namna ya kufika vituo vya huduma kwa upande wa walemavu wa miguu.
" ili uwafikie viziwi inatakiwa uwe na rasilimali fedha za kutosha, inategemea na jinsi sisi tunatafuta wafadhili mbalimbali. Mfano kwenye programu ya Afya ya uzazi lazima tuwaite wale wahusika kupitia kutoa taarifa kwa viongozi wa tawi kutusaidia kufikisha taarifa kwa walengwa" alisema afisa wa jinsia na maendeleo (CHAVITA) chama cha viziwi tanzania

   Changamoto kubwa

vikwazo ni vingi vinavyo wakumba wanawake walemavu licha ya jitihada za serikali na taasisi binafsa tofauti kuingia katika vita ya kutetea wanawake kuondokana na unyanyasaji wa kijinsi
Mawasiliano
Sikwamba shule za viziwi shule zipo hamna inchini ila changamoto ni namna ya hawa wanawake kufika na kujifunza, wengine wanakosa nafasi ya kujifunza kwa kukosa Ada au fedha ya kuwapelekea au familia zao kuona hawana umuhimu wa huyu mlemavu kwenda kujifunza lugha ya alama
Kwa kukosa elimu ya lugha ya salamander. Huyu mwanamke anakosa namna ya kujielezea iwapo atafanyiwaa  kitendo chochote cha ukatili

Mimba zisizotarajiwa na maambukiziya ya magonjwa ya zinaa.  

Kwa kukosa namna ya mawasiliano ya kuwawezesha Kupata elimu juu ya Afya zao wanawake wengi wenye ulemavu wamepitia hii changamoto na kutokupata namna ya matibabu mapema kwa kukosa elimu ya dhati juu ya magojwa ambukizi ya zinaa. Wanawake wenyeulemavu wamekosa namna ya kujitetea hata mbele ya Dora kwa makosa ya kubakwa na kunyanyasika. Haya ni maisha halisi ya hawa wanawake zaidi ni vijijini ambako elimu ya usawa haijawafikia.


Nk: Chavita inatoa msingi na ushauri kwa viziwi hakitoi misaada ya kisheria ila kinakuunganisha na vyombo mbalimbali vya kisheria

No comments:

Post a Comment